Saturday, September 8, 2018

KUKU AINA YA KROILER NI UTAJIRI WA HARAKA KWA WAFUGAJI WADOGO WADOGO

Image result for kuku aina ya kroila
KUROILER :
Asili ya kuku hawa wa (Kroiler) kuroiler ni kutokea nchini India
Hawa ni kuku wa kibiashara yaani ni kama broiler wa kienyeji. Wana kuwa kwa haraka sana miezi mitatu mpaka minne anakuwa yupo tayari kwa kuliwa na kuingizwa sokoni kama akipewa matunzo mazuri. Sifa ya kuku hawa ni kwamba wanataga vizuri

Kuku hawa kwa mwaka unaweza ukavuna mala tatu kwa makadrio ya miezi 4.

"Kwa mfano mwezi wa 1 ukiingiza Vifaranga bandani hadi mwezi 4 utawauza, mwezi wa 5 ukiingiza Vifaranga bandani hadi mwezi wa 8 utawauza , mwezi wa 9 ukiingiza Vifaranga bandani hadi mwezi wa 12 utawauza."

Kwahiyo ni mizunguuko 3 kwa mwaka mmoja.

kila Batch ukiuza kuku 1,000 kwa mwaka utakua umeuza kuku 3,000 kwa makadilio ya wastani.

Huku kuku wa kienyeji pure mizunguuko 1-2 kwa mwaka.


Sifa Za Kuku Aina Ya Kuroiler

•Wanakua haraka.
•Wanakadiriwa kuwa na uzito kati ya kilo 3 mpaka 3 na nusu wakiwa na umri wa miezi 4
•Wanavumilia magonjwa.
•Wanafugika aina zote za ufugaji ndani, nusu huria na huria kabisa.

Muhimu
Kuku aina ya  kuroiler wanafaa vizuri zaidi katika upande wa uzalishaji wa mayai na kwa ukuaji wa haraka.

FAIDA ZA UFUGAJI KUKU AINA YA KROILER.
Kuroilers huwa na faida zaidi kuliko kuku wetu wa ndani yaani wa kienyeji kwa ujumla.
Wanaweza kuishi chini ya hali hiyo tu kama moja ya kuku wa kienyeji, lakini uzalishaji wao ni wa juu sana ikilinganishwa na kuku wa ndani.
Kuroiler ni kuku ambao asili yake ni kutoka India inayojulikana kwa nyama yake tamu Mbali ya uwezo wa kuishi katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote hususani katika nchi zinazoendelea kama yetu.
Mara zote anazalisha mayai 150 katika mwaka kinyume na wetu wa asili, ambayo huzailsha mayai kati ya 40 na 50 katika kipindi cha mwaka
Katika ukomavu, uzito hufikia  3.5kg, na kuifanya kuwa ni kuku bora wa nyama uikilinganisha na kuku wengine wa nyama ambao hufikia uzito wa 2-2.5kg.

 

PAUL FABIAN KISENA
BSc. Agricultural economics and agribusiness
SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICURTURE (SUA)
kisenapaul@gmail.com
kaluluagribusiness@gmail.com
+255(0)683937375/0713014501

No comments:

Post a Comment

Habari zilizopita

KILIMO CHA KOROSHO

KILIMO CHA KOROSHO UTANGULIZI Korosho ni zao la biashara ambalo chimbuko lake ni Ureno na baadae mnamo karne ya 16 ndipo li...