Monday, September 10, 2018

KILIMO CHA MCHICHA

Mchicha


KILIMO CHA MCHICHA
Mchicha ni mojawapo ya mboga za asili ambayo hulimwa katika mikoa yote hapa nchini. Mboga hii ina vitamin A, C, na madini aina ya chokaa na chuma kwa wingi Majani ya mchicha huliwa baada ya kupikwa au kutengenezwa supu.

Mchicha IPO aina tatu
Kuna mchicha unaitwa gwasi ni mchicha wa kienyeji huu kuotesha kwake unasia kwenye kitalu kisha unakuja kungoa na kuotesha kwenye tuta liloandaliwa


Kuna mchicha unaitwa lishe huu unarusha kwenye tuta liloandaliwa na inachukua siku 21 kuvunwa mbegu yake kg 4000
Mbegu nyingine supa na yenyewe kama lishe ila lishe ndo inafanya vema sana.
Mbegu za mchicha zinaweza kusagwa na kupata unga unaoweza kutumika katika mapishi mbalimbali kama vile kutengeneza ugali, uji, chapati na maandazi. 

Hali ya hewa na udongo kwa  kwa ajili ya ulimaji wa kilimo hiki.
Mchicha unahitaji maji ya kutosha katika kipindi chake chote cha ukuaji hadi kuvuna. Vilevile mchicha huhitaji udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye kuhifadhi maji.

Utayarishaji wa shamba.
Tengeneza shamba la mchicha kwa kutifua ardhi na kulainisha udongo wenye kina cha sentimeta thelathini. Weka mbolea ya samadi debe moja katika kila mita moja ya mraba. Panda mchicha katika matuta yenye upana wa 90cm-100cm.

AINA ZA MBEGU
1. Amaranthus hybridus huu ni mchicha wenye majani mekundu na mbegu zake ni nyeusi.
2. Amarantus africana ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni ni nyeusi.
3. Amaranthus hypochondriacus ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni njano hasa 4.Mbegu zake hutumika kutengeneza uji wa watoto wachanga.
5. Amaranthus dubius ni mchicha wa kienyeji na Aspinosus ni mchicha wenye miba mingi.


UPANDAJI
1. Mchicha upandwe katika tuta kwa mistari yenye nafasi ya sentimita thelathini.
2. Funika mbegu kwa kutumia udongo uliolaini na tandaza nyasi kavu baada ya kupanda ili 3.kutunza unyevunyevu na toa matandazo baada ya siku tatu hadi tano tangu siku ya kupanda.
4. Pandikiza mchicha kwa nafasi ya sentimeta kumi na tano kwa ishirini.
5. Mwagilia maji ya kutosha.

Namna ya kudhibiti wadudu waaribifu.

Adui mkubwa wa mchicha ni wadudu aina ya mafuta au kitaalamu zaidi huitwa spinach aphids ambao hufyonza utomvu wa mchicha na kusababisha majani kujikunja , mchicha kusinyaa na kunyauka. Kudhibiti wadudu hawa mwagilia mchicha wako kutumia chombo kinachotoa maji mithili ya mvua kitaalamu kinaitwa "watering can" ili kuwadondosha wadudu hao.


Mavuno
Mchicha huwa tayari kuvunwa baada ya majuma 3 hadi 6 tangu kupandwa au kupandikizwa. Uvunaji huweza kuendelea kwa muda wa miezi 2 hadi 3 kutegemeana na namna utakavyoamua kuuvuna mchicha wako.

Kiasi cha mavuno

Kila mita moja ya mraba huzalisha kiasi cha 4kg hadi 5kg za mchicha. Hii inamaanisha kuwa utapata kiasi cha tani 20 hadi 40 kwa hekta moja ya mchicha.
NAMNA YA KUHIFADHI MCHICHA KWA SIKU NYINGI ZAIDI
Baada ya kuvuna funga mashina ya mchicha na weka katika chombo chenye maji kwa kufanya hivyo unaweza kuhifadhi mchicha kwa muda wa masaa 24 yaani siku moja.



Ili kuhifadhi mchicha kwa zaidi ya miezi 4 fanya kama ifuatavyo:-
1. Vuna mchicha wako kisha usafishe vizuri
2. Funga katika mafungu.
3. Chemsha maji mpaka yachemke.
4. Tumbukiza mafungu ya mchicha katika maji yanayochemka kwa muda wa dakika 1 hadi 2.
5. Kausha vizuri chini ya kivuli na utunze mchicha wako katika sehemu isiyo na unyevunyevu.


No comments:

Post a Comment

Habari zilizopita

KILIMO CHA KOROSHO

KILIMO CHA KOROSHO UTANGULIZI Korosho ni zao la biashara ambalo chimbuko lake ni Ureno na baadae mnamo karne ya 16 ndipo li...