Monday, September 10, 2018

UFUGAJI WA SAMAKI




UTANGULIZI
Ufugaji wa samaki unakua kwa kasi sana hapa nchini tanzania kutokana na kuonekana kua na faida sana. hivyo nimeamua leo nikupe elimu kidogo ambayo itakusaidia wewe mfugaji ambaye ungependa kujikita katika ufugaji huo, hivyo tue pamoja ili kujua mengi.
Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)
Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.
 

UTENGENEZAJI WA BWAWA
Kuna aina mbali mbali za kutengeneza mabwawa ya samaki inategemea na eneo, kiasi cha samaki unao taka kufuga, aina ya samaki na hali ya uchumi.
Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha. 

Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng’ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza
Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.
Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

UPANDIKIZAJI WA VIFARANGA/MBEGU ZA SAMAKI KATIKA BWAWA
Kabla vifaranga hawaja safirishwa ni vyema kuwatoa katika bwa kubwa wanalo ishi na kuwaweka katika vibwa vidogo vidogo  kati ya masaa 24 hadi 72 kuendana na umbali wa safari bila kuwapa chakula chochote kile.
  • baada ya kuwasafirisha mfugaji  atakiwi kuviweka kwenye bwa moja kwa moja ila inatakiwa maji yalio tumika katika kuwasafirisha yabadilishane joto na maji ya bwawa ambalo wataenda kuishi. hivyo mfugaji anatakiwa kuliweka kontena ambalo vifaranga wamo ndani ya bwawa ambalo wataishi kwa dakika 30 hadi 35 bila kuwafungulia, baada ya hapo kontena liina mishwe taratibu ili kuwezesha maji ya bwawa na yaliyo kwenye kontena kubadilishana na baadae vifaranga watatoka taratibu,
endapo hautafanya hivyo  unaweza kusababisha vifaranga vyote kufa kutokana na mabadiliko   ya joto ambayo yanaweza kutokea ghafla.
  • unatakiwa kusafirisha vifaranga wako mda ambao hali ya hewa inakua sio joto yaan mda wa jion na asubuhi ili kuwezesha vifaranga kuimili misukosuko ya safari na bila kupatwa na joto kali.
CHAKULA NA UTUNZAJI WA SAMAKI BWAWANI
  • Samaki hutakiwa kupewa chakula angalau mara 2 kila  siku  unatakiwa kuzingatia mda sahihi wa kuwapa chakula yaan asubuhi saa 3-4 na jion saa 9 -10 samaki upewa vyakula tofauti kulingana na aina. 
Tabia ya ulaji wa samaki
  1. samaki wanao kula nyama (sangara, kambale)
  2. samaki wanao kula mimea carps
  3. samaki wanao kula mchanganyiko (perege,sato na samaki wa maji ya chumvi mfano kibua)


TARATIBU ZA ULISHAJI WA SAMAKI

UMRI(wiki)

UZITO(gm)

KIASI CHA CHAKULA KWA SIKU (gm)
1-2
5-10
1
2-3
20-50
2
3-5
50-110
3
5-7
110-200
4
7 nakuendelea

200 na zaidi

5



kaluluagribusiness@gmail.com
Intagram: KALULUAGRIBUSINESS
Facebookpage: KALULU AGRIBUSINESS SOLUTIONS
0713014501 /0683937375

                                                

No comments:

Post a Comment

Habari zilizopita

KILIMO CHA KOROSHO

KILIMO CHA KOROSHO UTANGULIZI Korosho ni zao la biashara ambalo chimbuko lake ni Ureno na baadae mnamo karne ya 16 ndipo li...