Sunday, September 9, 2018

CHANJO NA KINGA ZA KUKU

CHANJO NA KINGA ZA MUHIMU KWA KUKU WA MAYAI, CHOTARA, KIENYEJI.
LAYERS 

1. Baada ya kuanguliwa

Chanjo ya Marek's 
Dawa HVT
Namna: sindano

2. Siku ya 2 hadi 6
KINGA ya Pullorum 
Dawa: Trimazine 30%  plus Vitamin 
Namna: Maji

3. Siku ya 7
Chanjo ya Mdondo/Kideri (Newcastle)
Dawa: Newcastle vaccine [LASOTA] 
Namna: Maji

4. Siku ya 14 
Chanjo ya Gumboro
Dawa: chanjo ya Gumboro
Namna: Maji

5. Siku ya 16 - 20
KINGA ya Koksidiosis (coccidiosis) 
Dawa: Trimazine 30% plus vitamin (Vitalyte itafaa) 
Namna: Maji

6. Siku ya 21
Chanjo ya Mdondo tena.. [Maelezo yapo kwa juu]

7. Siku ya 27 hadi 32 
KINGA: kuimarisha kinga ya mwili 
OTC 20% changanga na Amin'Total vitamin 

8. Siku ya 35 hadi 39
KINGA: Mafua
OTC 50% au CORDIX (ukiona kinyesi kina muharo kiasi) au Tylosine 75% changanya na Amin'Total. 

9. Siku ya 56 
Chanjo: Ndui 

10. Siku ya 60 hadi 64 (Rudia namba 7 hapo juu) 

11. Wiki ya 12 ( kati ya siku ya 64 hadi 70) 
Chanjo: Typhoid 

12. Wiki ya 13 (kati ya siku 85 hadi 91)
KINGA: minyoo

13. Wiki ya 15 
Ukataji wa midomo

14. Wiki ya 16 
KINGA ya kipindupindu 
OTC 20 YA SINDANO
Sindano kwenye nyama ya kifua

15. Wiki ya 17
KINGA ya mafua
Tylosine ya sindano
Sindano kwenye nyama ya kifua

16. Wiki ya 18
chajo ya Typhoid 

 Baada ya hapo, waache kuku.. Hakuna sindano tena... 

Chanjo zinazobaki ni 

(A) Mdondo/Kideri(Newcastle Vaccine) aina ya LASOTA

(B) Gumboro (IBD) 

(C) Minyoo
____
Hizi zote ni kila baada ya miezi mitatu mitatu..

ZINGATIA.

Chanjo ndio dawa pekee kwa kuku, kuku wakishaugua au kuanza kuonyesha dalili za ugonjwa inakuwa ni ngumu sana kuwatibu kwasababu magonjwa mengi ya kuku huambukizwa kwa virusi

No comments:

Post a Comment

Habari zilizopita

KILIMO CHA KOROSHO

KILIMO CHA KOROSHO UTANGULIZI Korosho ni zao la biashara ambalo chimbuko lake ni Ureno na baadae mnamo karne ya 16 ndipo li...