Sunday, September 9, 2018

KUKU AINA YA BLACK AUSTRALORP

Black Australorp
Kuku hawa wanastahimili mazingira tofauti, kama kuku wa kienyeji aliye zoeleka nchini Tanzania.

Na ni wazuri kwa ufugaji huria au nusu huria, kwa kuwaachia nje wajitafutie chakula wenyewe.

Ingawa wanajulikana kwa sifa yao ya utagaji mayai mengi, lakini kuku hawa wanafaa kwa nyama pia, kwani huwa na nyama nyingi sana (dual purpose chickens)

Asili ya jamii hii ya kuku ni Australia  kutoka Black Orpingtons wakitokea Uingereza; na lengo la kueneza mpango wa uzalishaji wa kuku hawa  ilikuwa ni kwaajiri ya kueneza uzalishaji wa mayai kwa wingi na nyama.

Kuku hawa huweza kumpatia mfugaji faida kubwa, kwani ni wazuri kwa biashara ya mayai na nyama pia.

Hawana sifa nzuri ya kulalia mayai, lakini akilalia hutotoa vifaranga vingi, na ni wazuri kwa uleaji wa vifaranga hivyo.

Utagaji wao wa mayai unakaribia ule wa kuku wa kizungu.

Kuku hawa ni wakubwa, wazito, na wanamvuto sana kuwaangalia. Wanapendeza pia kwa ufugaji mdogo, katika mazingira ya nyumbani.

Wana michirizi ya kijani pale wanapomulikwa kwenye mwanga mkali wa jua.

Kwa wastani Black Australorp, hufikisha mayai 250 kwa mwaka, wakiwa katika mazimgira mazuri.

Kuku hawa ni wapole na rafiki kwa binadamu.

Black Australorp ni wagumu, hawapati magonjwa mara kwa mara, hivyo basi huvumilia magonjwa ya aina nyingi, na hawachagui chakula. Wanakula vyakula wanavyo kula kuku wengine wa kienyeji.

Huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi mitano na nusu hadi sita.

Jogoo hufikisha kilo 3.5 – 5.0 na
Temba/hen hufikisha kilo 3.0 – 3.7

KALULU AGRIBUSINESS SOLUTIONS
"Tulime na Kufuga kisasa"

No comments:

Post a Comment

Habari zilizopita

KILIMO CHA KOROSHO

KILIMO CHA KOROSHO UTANGULIZI Korosho ni zao la biashara ambalo chimbuko lake ni Ureno na baadae mnamo karne ya 16 ndipo li...