FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU
Fursa katika ufugaji wa kuku
Fursa ni changamoto au matatizo yaliyotuzunguka. Kwa maana
nyingine ni vitu gani tunavipata kwa shida katika mazingira yetu ya
kawaida.
Tumekuwa tukipata shida sana kufahamu jinsi ya kujua fursa zilizotuzunguka kutokana
na kutojua neno fursa lina maana gani hasa kwa mapana yake. Tukija
katika sekta ya ufugaji wa kuku, fursa iliyopo ni changamoto
tunazokumbana nazo kila siku katika ufugaji wa kuku aina zote.
Tusilalamike kuwa hatuwezi kufanikiwa. Katika mazingira yetu kuku
kazoeleka kama utamaduni wa kila kaya ya kitanzania kuwa na kuku lakini
anachukuliwa kama mfugo wa kawaida asiye na faida yoyote, lakini kuku ni
fursa kubwa ambayo imetoa watu wengi kiuchumi. Tutumie nafasi
tuliyonayo kujikwamua kiuchumi.
Hizi ni faida za ufugaji wa kuku.
1. Kuanza na mtaji mdogo
Hii ni moja kati ya faida za
kuanzisha mradi wa kuku. Kwa kawaida mtu yoyote anaweza kuanzisha mradi
huu wa kuku kwa sababu hauhitaji mtaji mkubwa ili kuanza. Mfano kuku
mmoja ambaye ni mtetea ma jogoo mmoja unaweza kuanza kama mradi.
Changanuo ufuatao unaonyesha ni kwa jinsi gani. Mtetea mmoja na jogoo
unaweza kununua kwa elfu 25 kwa maana jogoo elfu 15 na mtetea 10, baada
ya mwezi mtetea atakuwa ameanza kutaga na ndani ya mwezi. Kipindi
amemaliza kutaga ukamuwekea mayai 10 na 15 ndani ya siku 21 atatotoa
vyote au 10. Vifaranga 10 ukawalea mpaka miezi 6 watakuwa kuku wakubwa
na baadaya hapo wataanza kutaga na kulalia na kupata vifaranga wengi na
ukaendelea kupata kuku wengi zaidi. Ndio maana unaweza kutumia mtaji
mdogo na baada ya kuwa na kuku wengi na kuanza kuuza.
2.Chanzo chan mapato.
Kuku ana bidhaa muhimu kama vile mayai, nyama, na kinyesi ambacho hutumika kama mbolea ya asili. Vyote hivi ni mahitaji ya binadamu
katika maisha ya kila siku. kupitia kufuga Kuku utapata fursa ya
kutengeneza pesa nyingi tu. Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri, kwa maana
kuwapa chanjo kwa wakati, chakula bora na kutibu magonjwa pindi
yakitokea. Kuku wa kienyeji aliyekoma anauzwa 15000, 20000, 25000, 30000
na kuendelea inategemeana na kuku mwenyewe. Tatizo kubwa tulilonalo
Watanzania hasa kwa kuku wa kienyeji kadhalaulika na kuonekana ni wa
kawaida lakini tukikaa kujua trei moja mayai ya kienyeji linauzwa 15000.
Je? Ukiwa unaweza kuzalisha trai 5 kwa siku utakuwa na shilingi ngapi.
Tuamke na kufanya ufugaji wa kuku kuwa wa uwakika.
3.Utawala wa mradi wa kuku ni rahisi.
Urahisi huu hauna
maana kuwa hakuna ugumu hapana ila maana kubwa ya hii pointi ni kwamba
hatakama ni mfanyakazi wa kuajiliwa utapata muda wa kufuatilia kwa
karibu maendeleo ya kuku wako. Mfano umeanza na mradi wako wa kuku 100
,umewafugia nyumbani kwa kawaida unatakiwa kujipangia ratiba. Kwamba
kabla ya kwenda kazi ni kufika bandani na kuwa hudumia kuku wako, hata
kama utamwachia kijana aendelee kuwa hudumia kipindi ukiwa kazini,
utakuwa unajua kuku wako wako salama. Pia jioni ukitoka kazini inabidi
upate muda wa kipitia bandani na kuona hali ilivyo na kupata mrejesho
kutoka kwa kijana uliyemwachia.
4.Soko la kuku ni kubwa Tanzania na nchi za nje pia.
Hili
swala ni fursa kubwa kwetu sisi vijana hasa ambao tumekuwa tukilalamikia kuhusu mambo ya ajira za serikali na mashirika binafsi. Lakini tazama watu wa
nje ya nchi na baadhi ya wenyeji wanaoingiza bidhaa za kuku kama,
vifaranga, kuku na mayai. Wakati nafasi ya kuzalisha hapa hapa tunayo ni
swala la maamuzi na kuacha kulalamikia serikali juu ya ajira. Vijana
ajira tunayo mikononi mwetu ni swala la kuchukua hatua. Uwezekano upo
kwa Tanzania kuanza kujihidumia yenyewe na kuanza kutoka nje ya mipaka
pia. Takwimu zinaonyesha bado hata nusu ya matumizi ya kuku kwa ndani ya
nchi, Cha msingi ni sisi kutafuta taarifa sahihi ili kuweza kufanya
maamuzi sahihi.
Fuatilia machapisho mbalimbali na semina zinazotolewa na vijana wazoefu katika sekta ya kilimo na ufugaji kutoka KALULU AGRIBUSINESS SOLUTIONS ili uweze kuthubutu kujiajiri kupitia mradi wa kuku.
TAMBUA
Mradi wa kuku ni benki hai.Benki hai ni namna ya kuhifadhi pesa yako kwa matumizi ya baadae. Sasa ufugaji wa kuku ni benki hai maana yake ukiwekeza pesa yako katika kuku itakuwa sehemu salama na itaongezeka kwa kadri unavyozidi kuzalisha kuku wengi. Benki hii ni tofauti na benki za kawaida kwa sababu hakuna gharama yoyote ya makato ya uendeshaji, hapa ni kuhakikisha pesa yako inakuwa ni jitihada zako kuhakikisha unazalisha kuku wengi
No comments:
Post a Comment