KILIMO CHA VITUNGUU
Utangulizi
Vitunguu
maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi Duniani zenye hali ya
hewani baridi ya wastani na joto kiasi.
Vitunguu
ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake. Tanzania vitunguu hulimwa
sana sehemu za Mang’ula, Mgeta na Singida.
Hata
hivyo vitunguu hustawi maeneo mengi ya Tanzania. Vitunguu vinaweza kulimwa
mwaka mzima endapo maji yanapatikana.
Vitunguu
vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin
C na vitamin E
.
HALIJOTO
Joto
linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa
mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata
mazao kidogo.
AINA YA UDONGO
Vitunguu
huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba,usiotuamisha maji na usionata
sana.
Hufanya
vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio
mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima.
Udongo
mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga.
Umwagiliaji
ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari
sana kipindi cha ukuaji.
Epuka
matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na
shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu.
UPANDAJI WA VITUNGUU
Kabla
ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na
mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja.
Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza
kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na
sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari
EPUKA
Kununua
mbegu za mitaani, kuzidisha sana mbolea na umwagiliaji usio na mpangilio kwani
husababisha vinguu kuzaa pacha.
Pia
epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za
nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani.
KITALU CHA VITUNGUU
Ni
muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu
kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa
penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini.
AINA ZA VITUNGUU VINAVYOLIMWA NCHINI
TANZANIA
·
Red
Creole
·
Bombay
Red
·
Hybrid
F1
UANDAAJI WA MBEGU
Uchaguzi
wa mbegu bora ni muhimu sana katika uzalishaji miche yenye afya bora na yenye
uzalishaji mazao mengi na yaliyo bora. Mbegu bora lazima ziwe na sifa
zifuatazo;
1.
Mbegu safi zisizo na mchanganyiko
2.
Uotaji zaidi ya 80%
3.
Chanzo sahihi cha uzalishaji mbegu
4.
Tarehe ya uzalishaji mbegu isizidi mwaka mmoja
5.
Chagua mbegu yenye soko kulingana na wakati
6.
Hekta moja inatosha mbegu 3.5 hadi 4kg
UHAMISHAJI WA MICHE YA VITUNGUU
KUTOKA KITALUNI KWENDA SHAMBANI
Zoezi
la uhamishaji wa miche ya vitunguu hufanywa wakati miche imefikia umri wa wiki
7- 9.
Pia
miche hiyo iwe imefikia unene wa shingo yakitunguu ukubwa wa 1/2 ya penseli au
3/4 penseli na wakati huo miche iwe imefikia urefu wa 15cm, Pia shina la
kitunguu unapanda kwenye shimo lenye urefu wa 5cm.
NAMNA YA UTUNZAJI WA SHAMBA
Inashauriwa
kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua ili kuongeza ruba ya
ardhi na pia kuzuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu
kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuia utuamishaji wa maji na mlipuko
wa magojwa ya miche. Pia inashauriwa kung’oa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.
MATUMIZI YA MBOLEA
Vitunguu
hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi au mboji iliyoiva
vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo7.5 -12
kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1.
UMUHIMU WA PALIZI KWENYE VITUNGUU.
Palizi
kwenye zao la vitunguu ni muhimu sana kwa sababu ya kuongeza kipato. Kwani
magugu yanauwezo wa Mkubwa mno wa kuchukua virutubisho vingi kwenye ardhi
kuliko vitunguu, hivyo hupelekea vitunguu kupunguza uzaaji nzuri na kusababisha
upungufu wa mavuno kutokea. Magugu hayo yanaweza kudhibitiwa kupitia jembe la
mkono, ung'oaji magugu kwa kutumia mkono, au kutumia madawa ya kuja wadudu.
MAGONJWA YA VITUNGUU MAJI
Kuna
magonjwa mbalimbali yanayosumbua zao la kitunguu, lakini magonjwa makubwa
yanayojitokeza sana katika ZAO hili ni pamoja na ;
1. Ukungu
wa unga (powdery mildew) na wa chini (downy mildew).
Magonjwa
haya hushambulia majani ya mimea shambani na hata miche michanga. Katika majani
huonekana vidoa vyeupe hasa kwenye majani makuu ya mimea michanga. Kwani
ugonjwa huu hutokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu za baridi au nyakati
za baridi. Ugonjwa juu unaweza kudhibitiwa na dawa kama mancozeb.
2. Ugonjwa
wa doa la pinki (Purple blotch)
Ugonjwa
huu huanza kama doa dogo linalozama ndani ya nani na kisha linaongezeka ukubwa
na kufanya ranging ya pinki. Kiini cha ugonjwa juu huanzia kwenye mbegu na pia
hubakia kwenye maozo ya majani ya vitunguu.
Udhibiti
wa ugonjwa juu ni kulima Kilimo cha kubadilisha mazao (crop rotation). Pia
tunaweza kudhibiti ugonjwa huu kwa kuzuia kutuama kwa maji shambani, msongamano
wa mazao shambani na matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate na potassium
hupunguza kuenea kwa ugonjwa juu.
3.
Kuoza kwa vitunguu (bulb rots)
Ugonjwa
juu ni hatari zaidi huweza kutoka shambani au wakati wa hifadhi ghalani.
Ugonjwa juu huweza kujitokeza zaidi sehemu zenye joto na kutuamisha maji.
Udhibiti
wake kuhakikisha shambani hakuna hali ya kutuamisha maji na pia kwenye ghala
kuna kuwa na hali nzuri ya mzunguko wa hewani.
WADUDU WANAOSHAMBULIA ZAO LA
KITUNGUU.
Kati
ya wadudu wasumbufu wa zao la kitunguu ni pamoja na ;
1. Utitiri
wa vitunguu (Onion thrips)
Hawa
ni wadudu wadogowadogo sana ambao hula kwa kukwaruza juu ya jani na kunyonya
majimaji ya kwenye mmea. Hali ambayo hupelekea kutoka kwa mikwaruzo meupe
kwenye majani ya vitunguu, hali ambayo ikizidi hupelekea kunyauka kwa majani ya
mmea na hatimaye majani hayo kuanguka, vile vile husababisha kupungua kwa
ukubwa wa vitunguu. Tatizo la hao wadudu hujitokeza zaidi nyakati za ukame
kuliko wakati wa unyevu.
2. Bungua
weupe (white grub)
Huyu
ni aina ya funza Mkubwa hutaga mayai yake kwenye uozo wa majani na samadi,
hivyo mashamba ya vitunguu ambayo hapo kwenye maeneo hayo au karibu na maeneo
ya jinsi hiyo yapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kukabiliwa na tatizo hilo la
hao wadudu.
Kwa
wadudu hao hushambulia mizizi ya mmea wa kitunguu na kusababisha mmea huo
unyauke, na hatimaye hufa. Wadudu hao tunaweza kuwa punguza kwa kutifulia
shamba na kuwaweka wazi wadudu
UVUNAJI
Vitunguu
huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka
kwa majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa
shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu
hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza
kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe
kwenye nyuzi joto chini ya 4.4 °C ama juu ya nyuzijoto 25°C ili visiharibike.
UUZAJI
Vitunguu
ni zao lenye bei nzuri ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa
kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri.
Kama
vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo Ekari moja huzaa gunia 70-90
sawa na kg 7000-9000. Kama akipata soko la uhakika mkulima anaweza kupata hadi
13.5 milioni kwa msimu mmoja
1. Kuongea kipato cha mkulima
2. Chanzo cha ajira
3. Huongeza pato la Taifa na kuchangia katika maendeleo ya Taifa
4. Hutumika kama mboga na kiungo
For
more info:
No comments:
Post a Comment